MKASA WA MTETEMEKO WA ARDHI HUKO UCHINA
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon, ameipongeza Nchi ya Uchina kwa uongozi wake mwema kutokana na mtetemeko wa ardhi wa hivi karibuni katika jimbo la
more
ichuan.
Alikuwa akiongea katika mji wa Yingxiu ambao umeadhirika sana na mtetemeko huu wa ardhi. Vile vile, waziri mkuu wa Uchina Wen Jiabao amesema ya kuwa, kufikia sasa vifo vya watu vimepita elfu sitini na vyaweza kufikia elfu themanini.
Bwana Ban amesema kuwa umoja wa mataifa uko tayari kutoa misaada zaidi.
Hapo mbeleni, afisa wa kichina alisema kuwa mitambo hamsini ya kinuklia ilikuwa imezikwa. Taarifa kutoka kwa waziri mdgo wa mazingira Wu Xiaoqing inasema kuwa, thelathini na tano kati ya mitambo hii imezikwa katyika mawe na majumba mabovu. Ingawa Bwana Wu amedhibitisha kuwa hakuna mitambo yoyote ya kinuklia iliyofuja, wanayansi wanasema ya kuwa huenda ikawa madini ya kinulkia yalitoka katika hospitali viwanda ama vituo vya kufanyia uchunguzi lakini si vifaa ama vyombo vya kivita
Bwana Ban ambaye amezuru Burma anatafuta misaada zaidi kwa wahasiriwa wa kibunga Nargis. Jumamosi iliyopita alikifungua rasmi kituo cha misaada cha kibunga huko Thailand.
Karibu na Sichuan, kulikotokea mtetemeko wa ardhi, aliwapongeza wenyeji wa Yingxiu, kwa jitihada waliozoweka kuwashughulikia wahasiriwa.
“Serikali ya Uchina iemjaribu iwezavyo na imeonyesha uongozi na jitihada katika mkasa huu,” Alisema Bwana Ban. Aliendelea kusema kuwa watu wote duniani wanaiunga na wataisaidia Uchina katika mkasa huu.
“Tukiungana, tutashida,” Alinakiliwa na ripotikutoka kwa APNA [Associated Press News Agency] “ Dunia nzima iko nyuma yenu na inawaunga.”
Zaidi ya watu milioni tano wameachwa bila makao kwasababu ya makasa huu.
Ijumaa, katika jimbo liliadhirika zaidi la Li Chengyuu, gavana msaidizi aliitisha misaada zaidi ya mahema na kufumbua rasmi mpango wa miaka mitatu wa kujenga jimbo hilo.
Viongozi wa kichina pia wamebuni kikapu cha fedha cha kuwezesha ujenzi kitakachogharimu dola bilioni kumi.
Serikali pia imetoa ombi kwa benki humo nchini kufutilia mbali madeni ya wahasiriwa ili kuiimarisha tena uchumi wa Sichuan.
less